Isaiah 30:1-3

Ole Wa Taifa Kaidi


1 a Bwana asema,
“Ole kwa watoto wakaidi,
kwa wale wanaotimiza mipango ambayo si yangu,
wakifanya makubaliano, lakini si kwa Roho wangu,
wakilundika dhambi juu ya dhambi,

2 bwale washukao kwenda Misri
bila kutaka shauri langu,
wanaotafuta msaada wa ulinzi wa Farao,
watafutao kivuli cha Misri kwa ajili ya kimbilio.

3 cLakini ulinzi wa Farao utakuwa kwa aibu yenu,
kivuli cha Misri kitawaletea fedheha.
Copyright information for SwhKC